Lugha asilia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lugha asilia ni lugha ambayo ilikua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani ambao watu wake wanaiongea kama lugha mama. Ni kinyume cha lugha ya kuundwa (lughaundwe).

Mara nyingine lugha asilia maana yake ni lugha yoyote ambayo inaweza kuzungumzwa na watu, huku lugha za kompyuta na za kuandaa programu zinaitwa lugha za kuundwa.

Mara nyingine tena lugha asilia ni lugha ambayo mtu huzaliwa nayo au huikuta baada ya kuzaliwa. Hata hivyo lugha asilia huwa chimbuko la watu fulani katika jamii na hutofautisha jamii moja na nyingine. Mara nyingi ni sehemu ndogo tu ya jamii ndiyo huwa na lugha asilia yaani kila ukoo au kabila huwa na lugha yake ya asili.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha asilia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.