Hoteli
Mandhari
Hoteli (kutoka neno la Kiingereza hotel linalotokana na lile la Kifaransa hôtel ambalo, sawa na neno "hospitali", lina asili katika Kilatini hospes, yaani mgeni) ni jengo kubwa lenye vyumba vingi, ambapo watu wanaweza kulala wakati hawapo nyumbani.
Wenye sehemu hizo wanakodisha chumba kwa siku yoyote. Wanatoa vyumba vya kulala, na kwa kawaida hata chakula, hatimaye kwa ajili ya huduma hizo hutaka pesa, ambazo kiasi chake hutegemea ubora wa jengo.
Pia kuna hoteli ambapo mikutano hufanyika.
Aina za hoteli
[hariri | hariri chanzo]Aina za hoteli hulinganishwa na wingi wa vyumba na eneo ambalo hoteli hupatikana.
- Resort hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na mito, maziwa, milima, pembezoni mwa bahari au katika kisiwa, [1]
- Inn hotel ni aina ya hoteli ambazo mara nyingi hutoa huduma za malazi na kifunguakinywa. [2]
- Airport hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu kabisa na viwanja vya ndege na mara nyingi hutoa huduma zake kwa wasafiri wa ndege. [3]
- Motel hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na barabara kubwa na huwa na vyumba vichache kutoa huduma sana kwa madereva wa magari ya watalii. [4]
Aina za vyumba vya hoteli
[hariri | hariri chanzo]Aina za vyumba hutazamwa kulingana na aina au idadi ya vitanda vilivyomo ndani yake.
- Single room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya kulala mtu mmoja tu[5]
- Double room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya watu wawili na huwa na kitanda kimoja kikubwa.
- Twin bed ni aina ya chumba chenye vitanda viwili vilivyo karibu, wakati mwingine anaweza kulala mtu mmoja katika aina hii.
- Suite room ni aina ya chumba kikubwa kilicho na sehemu ya kulala pamoja na sebule.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Resorts, Different Resorts, Types of Resorts | Elite Cruises and Travel". Elite Cruises and Travel | Attentive Service | Deluxe Land Tours | Custom Itineraries | Luxury Travel (kwa American English). 2019-08-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-05. Iliwekwa mnamo 2020-02-05.
- ↑ "Difference Between Hotel and Inn | Difference Between" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-02-05.
- ↑ "Why is an Airport Hotel Different from the Normal Hotels?". Global Hospitality Portal (kwa American English). 2017-02-11. Iliwekwa mnamo 2020-02-05.
- ↑ "Motel - Definition Glossary for Hotel Revenue Management Terminology". Hotel Management Company - Hospitality Group - Xotels Ltd. (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2020-02-06.
- ↑ "Single room definition and meaning | Collins English Dictionary". www.collinsdictionary.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-02-07.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hoteli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |