Kitanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Kitanda (maana)

Kitanda cha Waswahili

Kitanda ni samani ya kulala au kusinzia.

Asili ya neno "kitanda" ni zizi la "-tanda".

Katika utamaduni wa Waswahili kitanda ni samani kubwa. Ina kiunzi au fremu ya ubao, yenye vitakizo viwili upande wa kichwa na mguuni vinavyoshikwa kwa mifumbati kila upande. Yote inakaa juu ya matendegu (miguu ya ubao) manne. Nafasi kati ya mifumbati inafumaniwa kwa kamba, usumba wa nazi au nyasi. Juu ya hii huwekwa mkeka au godoro. Vitakizo mara nyingi hupambwa kwa vioo vya rangi au vyenye picha. Kiunzi cha juu kinaweza kufunikwa kwa vitambaa au chandarua.