Nenda kwa yaliyomo

Gisenyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pembezoni mwa Ziwa Kivu katika mji wa Gisenyi.
Taxi huko stesheni.
Rammani ya Gisenyi

Gisenyi au Kisenyi ni mji ulioko magharibi mwa Rwanda na unapatikana katika wilaya ya Rubada. Mji unajumuisha na Goma na upo mpakani wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mwaka, 2005 ulikuwa na wakazi 83,623.

Pia umepitiwa na Ziwa Kivu ambalo linapelekea uwepo wa michezo ya majini, hoteli. Pia mji huu ni makazi ya kiwanda cha Bralirwa ambacho hutegeneza vinywaji baridi kama Primus, Guinness, Amstel na kuna kiwanda kama Coca-Cola ambacho nacho hufanya kazi ya kuzalisha vinywaji baridi.

Gisenyi ni mji mdogo ukilinganisha na mji wa jirani Goma lakini mji wa Gisenyi umeendelea kwa kiasi kikubwa mnamo mwaka 2011 ambapo kulikuwa na barabara na huduma nyingine nyingi.

Mlima Nyiragongo ni mlima wa volkano kati ya Gisenyi na Goma ambao uliwahi kulipuka mwaka 1977, tena mwaka 2002 na mji uliathiriwa kwa 15% kati ya 40% ya janga hilo lakini hawatodhurika sana endapo janga hilo litatokea tena.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gisenyi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.