Transparency International

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Transparency International (kifupi TI) ni Shirika Lisilo la Kiserikali la kimataifa lenye shabaha ya kupambana dhidi ya rushwa na hongo kote duniani. Makao makuu yako Berlin (Ujerumani).

Shirkia liliundwa mwaka 1993 huko Berlin na Peter Eigen na marafiki zake. Eigner aliwahi kuwa mkurugenzi wa Benki ya Dunia akaanzisha TI kutokana na maarifa yake kazini.

Chanzo cha TI[hariri | hariri chanzo]

Eigen alipata hoja la kuanzisha TI alipoongoza kamati ya ukaguzi wa miradi iliyolipiwa na msaada wa kimataifa nchini Kenya. Alitambua ya kwamba mara nyingi miradi yenye gharama kubwa zilipewa kipaumbele na mashirika yanayotoa misaada lakini pia na serikali za nchi zinazopokea misaada hata kama miradi hii haina faida kubwa kwa watu wanaolengwa na miradi pia hata kama miradi hii inaongeza madeni ya nchi inayopokea. Kamati ilitambua ya kwamba maafisa wa pande zote mbili yaani upande wa kutoa fedhas pia upande wa kupokea mara nyingi walipendelea miradi ghali kwa sababu za faida zao binafsi. Hasara ilikuwa wazi kwa nchi zinazopokea misaada kwa sababu madeni yao huongezeka inayopaswa kulipiwa baadaye. Hasara ilionekana pia upande wa nchi zinazotoa pesa ya misaada kwa sababu pesa ya umma hutumiwa kwa faida za binafsi ya makampuni makubwa wanaouza bidhaa na huduma kwa bei ya juu wakizuia msaada kufika kwa watu maskini wanaotakiwa kufaidia na msaada ule.

Kamati ilijifunza pia ya kwamba rushwa ilikubaliwa kwa namna fulani katika nchi ambako sheria ya kodi zilikubali gharama za "kusahalisha" na kuwezesha makampuni kukata gharama hizi katika deni la kodi hivyo kuruhusu hali halisi rushwa kufidiwa na idara ya kodi.

Ramani ya matokeo ya 2006 ya taarifa kuhusu rushwa duniani: "Index of perception of corruption"
nyekundu: kiwango cha juu; buluu: kiwango cha chini

Hivyo kundi la watu wa siasa na biashara kutoka nchi za Ulaya na kutoka Afrika na Asia walianzisha shirika la TI. Walifaulu kuamsha serikali nyingi pamoja na shirika kubwa za kimataifa kuhusu maovu ya rushwa. TI imesababisha mabadiliko ya sheria katika nchi mbalimbali.

Taarifa ya kimatifa kuhusu rushwa (Corruptions Perceptions Index)[hariri | hariri chanzo]

TI imejulikana hasa kutokana taarifa zake za kila mwaka kuhusu kiwango cha rushwa katika nchi za dunia (Corruptions Perceptions Index). Taarifa hii hutolewa kutokana na maoni ya wataalamu na wafanyabiashara wanaoulizwa jinsi wanavyoona kiwango cha rushwa katika nchi fulani.

Taarifa hii hupingwa mara nyingi kwa sababu haitumii takwimu halisi ila tu mawazo na maoni ya watu wanaochaguliwa na TI. Ila tu hadi sasa hakuna njia bora inayojaribu kupima kiwango cha rushwa. Kwa hiyo wengi wameikubali kama onyo au mshale (indiketa) ya tatizo hili.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]