Mlango wa bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlango wa bahari ya Gibraltar kati ya Afrika na Ulaya huuunganisha Mediteranea na Atlantiki

Mlango wa bahari (pia: mlangobahari, ing. strait) ni mahali ambako magimba mawili ya nchi kavu hukaribiana kwa pwani zao na kuacha nafasi kwa ajili ya bahari.

Mlango wa aina hii mara nyingi ni njia muhimu ya mawasiliano, usafiri na biashara. Milango ya bahari ina pia umuhimu wa kijeshi kwa sababu anayetawala mlango ana nafasi ya kuzuia au kuruhusu wengine watumie ama wasitumie njia hiyo.

Mifano ya milango ya bahari ni kama vile:

Jina la mlango wa bahari Iko kati ya Inaunganisha bahari za
Mlango wa Gibraltar Moroko na Hispania (Afrika/Ulaya) Atlantiki - Mediteranea
Bab el Mandeb Jibuti na Yemeni (Afrika/Asia) Bahari ya Shamu na Bahari Hindi
Mfereji wa Kiingereza Uingereza na Ufaransa (Ulaya) Atlantiki na Bahari ya Kaskazini
Mlango wa Malakka Malaysia na Sumatra / Indonesia (Asia) Bahari Hindi na Bahari ya Uchina
Bosporus na Dardaneli Uturuki upande wa Ulaya na
Uturuki upande wa Asia
Mediteranea na Bahari Nyeusi
Mlango wa Bering Alaska (Marekani) na Siberia (Urusi)
Amerika ya Kaskazini na Asia
Pasifiki na Bahari ya Aktika
Skagerak na Kattegat Denmark na Norwei / Uswidi (Ulaya) Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki