Mlango wa Malakka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mlango wa Malakka (mviringo nyekundu)
Map of the Strait of Malacca-de.jpg

Mlango wa Malakka ni mlango wa bahari kati ya Malaysia na kisiwa cha Sumatra (Indonesia) mwenye urefu wa 800 km. Sehemu yake nyembamba ni 2,8 km pekee. Unaunganisha Bahari Hindi na Bahari ya Uchina ambayo ni bahari ya kando la Pasifiki.

Bandari muhimu zaidi ni Malakka (Malaysia) na Singapur.

Ni kati ya njia za bahari zinazotumiwa zaidi duniani. Kila siku meli 2,000 zinapita humo, kwa jumla 20% - 25 5 ya biashara yote ya baharini inategemea mlango huu wa bahari.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • Maleisie.be - Meer over de regio en geschiedenis van Malakka (NL)