Mlango wa bahari
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mlangobahari)
Mlango wa bahari (pia: mlangobahari, ing. strait) ni mahali ambako magimba mawili ya nchi kavu hukaribiana kwa pwani zao na kuacha nafasi kwa ajili ya bahari.
Mlango wa aina hii mara nyingi ni njia muhimu ya mawasiliano, usafiri na biashara. Milango ya bahari ina pia umuhimu wa kijeshi kwa sababu anayetawala mlango ana nafasi ya kuzuia au kuruhusu wengine watumie ama wasitumie njia hiyo.
Mifano ya milango ya bahari ni kama vile:
Jina la mlango wa bahari | Iko kati ya | Inaunganisha bahari za |
---|---|---|
Mlango wa Gibraltar | Moroko na Hispania (Afrika/Ulaya) | Atlantiki - Mediteranea |
Bab el Mandeb | Jibuti na Yemeni (Afrika/Asia) | Bahari ya Shamu na Bahari Hindi |
Mfereji wa Kiingereza | Uingereza na Ufaransa (Ulaya) | Atlantiki na Bahari ya Kaskazini |
Mlango wa Malakka | Malaysia na Sumatra / Indonesia (Asia) | Bahari Hindi na Bahari ya Uchina |
Bosporus na Dardaneli | Uturuki upande wa Ulaya na Uturuki upande wa Asia |
Mediteranea na Bahari Nyeusi |
Mlango wa Bering | Alaska (Marekani) na Siberia (Urusi) Amerika ya Kaskazini na Asia |
Pasifiki na Bahari ya Aktika |
Skagerak na Kattegat | Denmark na Norwei / Uswidi (Ulaya) | Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki |