Mlango wa Bering

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mlango wa Bering unavyoonekana kutoka angani
Ramani ya mlango wa Bering

Mlango wa Bering (Kirusi: Берингов пролив; Kiing.:Bering Strait) ni mlango wa bahari na mahali pa kukaribiana kati ya Alaska upande wa Amerika ya Kaskazini na Siberia upande wa Asia.

Mlango wa Bering una upana wa takriban 92 km na kina cha 30 hadi 50 m pekee. Unaunganisha bahari ya Aktiki na Pasifiki.

Jina limetokana na Vitus Bering aliyekuwa Mdenmark katika urumishi wa Kaisari wa Urusi aliyevuka mlnago huu mwaka 1728.

Maeneo kando la mlango Bering pande zote mbili yana watu wachache kwa sababu ya mazingira baridi.

Kufuatana na nadharia za wataalamu wa historia hapa palikuwa mahali pa kuvuka kwa watu wa kwanza kutoka Asia kwenda Amerika. Inafikiriwa ya kwamba wakati wa Enzi ya Barafu miaka 10,000 iliyopita mlango ulikuwa kavu ukapitika kwa miguu.