Rabat
Jiji Casablanca, Morocco | |
Mahali pa mji wa Rabat katika Moroko |
|
Majiranukta: 34°1′20″N 6°50′4″W / 34.02222°N 6.83444°W | |
Nchi | Moroko |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 627 000 |
Tovuti: http://www.rabat.ma/ |
Rabat (Kiarabu الرباط Ar-Ribat) ni mji mkuu wa Moroko na mji mkubwa wa pili nchini baada ya Casablanca ikiwa na wakazi 1,622,860 (2004) pamoja na Sale. Jina lenyewe la "ribat" linadokeza kwa asili ya mji kuwa boma la kijeshi.
Rabat iko mwambanoni wa Atlantiki kwenye mdomo wa mto Bou Regreg. Ng'ambo ya mto iko Sale ambayo ni mji pacha. Miji yote miwili ina viwanda vya nguo, vyakula na za ujenzi. Utalii pamoja na mabalozi ya nchi nyingi walioko Rabat kwa mfalme wanaongeza misingi ya uchimu wa mji.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mji wa kwanza katika eneo la Rabat ya leo ulikuwa Chellah. Maghofu yake ni kando la mji wa kisasa ufukoni wa mto Bou Regreg. Mwaka 40 KK Waroma wakauvamia na kkufanya mji wa Kiroma wa Sala Colonia. Kuanzia mnamo mwaka 250 BK mji ulikuwa chini ya watawala wa Kiberber.
Hadi mwaka 1146 mji wa kale ulikuwa umeshapungua sana labda hata bila watu kwa sababu mwaka ule mtawala wa Wamuwahid Abd al-Mu'min alijenga "ribat" yaani boma la mpakani kilomita kadhaa kutoka majengo ya Chellah yaliyotumika kama machimbo ya mawe ya kujengea.
Mjukuu wake Ya'qub al-Mansur alihamisha mji mkuu wake hapa. Alianzisha majengo makubwa lakini alikufa labla ya kuyatimiza. Mnara wa Hassan umebaki hadi leo. Baada ya kifo chake makao ya mfalme yalihamishwa kwenda Fez mji ulipungua hadi kuwa na nyumba pekee yenye watu 100 mwaka 1515 BK.
Katika karne ya 17 BK miji ya Rabat na Sale ilijitegemea kuwa pamoja dola ndogo la Jamhuri ya Bou Regreg 1627 hadi 1818. Maisha ya wenyeji ilikuwa hasa uharamia baharini wakishambulia hasa jahazi za Wakristo hadi kuingizwa kwa eneo katika Ufalme wa Moroko.
Wafaransa walipovamia Moroko 1912 na kuifanya nchi lindwa wakapeleka makao makuu tena Rabat kwa sanbabu za usalama. Sultani Moulay Yusef aliwafuata na kuhamisha ikulu yake Rabat vilevile.
Wakati wa uhuru mwaka 1956 Mfalme Mohammed V aliamua Rabat iwe mji mkuu wa kudumu.
Wenyeji wa Rabat
[hariri | hariri chanzo]- Younes El Aynaoui (* 12.09. 1971), mcheza tennis
- Dominique de Villepin (* 14.11. 1953), Waziri Mkuu wa Ufaransa (2005/6)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Travel in Rabat-History Ilihifadhiwa 10 Novemba 2005 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Entry in Lexicorient Ilihifadhiwa 6 Februari 2005 kwenye Wayback Machine.
- rabatcit Ilihifadhiwa 25 Julai 2021 kwenye Wayback Machine. for more information