Bikira Maria wa Rozari


Bikira Maria wa Rozari ni jina mojawapo linalotumika kwa Bikira Maria kuhusiana na rozari yake.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 7 Oktoba[1], siku ambayo mwaka 1571 jeshi la majini la Wakristo lilifaulu kushinda lile la Waturuki Waislamu katika mapigano ya Lepanto, karibu na Ugiriki.
Ushindi huo haukutegemewa, ila uliombwa na Wakatoliki wa Ulaya nzima kwa Rozari, kama alivyoagiza Papa Pius V[2][3]. Mjini Roma mwenyewe aliongoza maandamano ya ibada kwa ajili hiyo.
Matokeo yake yakawa ya kudumu: Waturuki hawakuweza kuteka Ulaya magharibi[4] wala kwenda Amerika kupitia bahari ya Atlantiki.
Basi, Papa alianzisha sikukuu ya kila mwaka kusherehekea ushindi huo.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Chesterton, Gilbert.Lepanto, Ignatius Press, 2004, ISBN 1-58617-030-9
- ↑ Butler's Lives Of The Saints (April) by Alban Butler (1999) ISBN 0-86012-253-0 page 222
- ↑ Melleuish, Gregory. "The significance of Lepanto", Quadrant, April 1, 2008. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-06-29. Iliwekwa mnamo 2016-09-16.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
![]() |
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Rozari kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |