Ziara ya Bikira Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani wa Kiorthodoksi katika kanisa la Mt. George huko Kurbinovo, Masedonia Kaskazini.

Ziara ya Bikira Maria (pia: Maamkio) ni ile iliyofanywa na Mama wa Yesu, alipokuwa mjamzito tangu siku chache, kwa Elizabeti, aliyekuwa na mimba ya miezi sita katika uzee wake (Lk 1:39–56[1][2]). Lengo lilikuwa kumhudumia hadi ajifungue mtoto, Yohane Mbatizaji, miezi mitatu baadaye[3][4].

Kadiri ya Injili, walipokutana tu, Roho Mtakatifu alimjaza kwanza Yohane Mbatizaji awe nabii, tena zaidi ya nabii (Math 11:9), naye aliruka kwa shangwe tumboni mwa mama yake, tena Elizabeti mwenyewe aliyetambua ujauzito wa Maria na hivyo kumpongeza kuwa mbarikiwa kuliko wanawake wote na mwenye heri kwa kuwa alisadiki kwamba aliyoambiwa na Bwana yatatimia.

Akiitikia unabii wao, Maria alimtolea Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa maarufu kwa jina la neno lake la kwanza katika Kilatini, Magnificat.

Tukio hilo la kusisimua linaadhimishwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo tarehe 31 Mei[5][6] au 2 Julai[7] katika Ukristo wa Magharibi na 30 Machi [8] au Jumapili mojawapo ya Majilio [9] katika Ukristo wa Mashariki.

Katika Rozari linakumbukwa kama fumbo la pili la furaha[10].

Pia limekuwa asili ya kazi nyingi za huruma na sanaa ya Kikristo.

Habari katika Injili[hariri | hariri chanzo]

Siku zile Mariamu aliondoka, akaenda upesi eneo la milimani katika mji wa Yuda; Aliingia katika nyumba ya Zakaria na kumsalimia Elizabeti. Ikawa, mara Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka kwa furaha; na Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu; na akasema kwa sauti kuu, akasema: «Umebarikiwa wewe katika wanawake na mzao wa tumbo lako amebarikiwa; na anijilie wapi mama wa Bwana wangu? Kwa maana, mara sauti ya salamu yako ilipofika masikioni mwangu, mtoto tumboni mwangu aliruka kwa furaha. Mwenye furaha yule ambaye ameamini kwamba yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana yatatimizwa!” (Injili ya Luka 1:39-45)

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Ray, Steve (October 2005). "Mary, the Ark of the New Covenant". This Rock 16 (8). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 May 2016. Iliwekwa mnamo 31 May 2016.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "Lesson Three: The Ark of the New Covenant – Lesson – St. Paul Center". stpaulcenter.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-05. Iliwekwa mnamo 2020-05-17. 
  3. Holweck, Frederick. Visitation of the Blessed Virgin Mary. The Catholic Encyclopedia. Vol. 15. New York: Robert Appleton Company, 1912. 11 October 2013
  4. Samaha S.M., Br. John M. The Visitation of the Blessed Virgin Mary Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.
  5. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 1969), p. 93
  6. Martyrologium Romanum
  7. "The Calendar". 16 October 2013. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-22. Iliwekwa mnamo 2020-05-17.  Check date values in: |date= (help)
  8. Frary, Lucien J. (2013). "Russian Missions to the Orthodox East: Antonin Kapustin (1817–1894) and his World". Russian History 40 (1): 133–151. doi:10.1163/18763316-04001008. 
  9. "The Holy Virgin Mary in the Syrian Orthodox Church". 14 February 2010.  Check date values in: |date= (help)
  10. "Joyful Mysteries (Without Distractions)". Rosary Center - Home of the Rosary Confraternity (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-11-17. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ziara ya Bikira Maria kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.