Nenda kwa yaliyomo

Kuzaliwa kwa Bikira Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya kuzaliwa kwa Mama wa Mungu.

Kuzaliwa kwa Bikira Maria ni sikukuu inayoadhimishwa tarehe 8 Septemba katika Kanisa Katoliki[1] na vilevile katika makanisa ya Waorthodoksi, ambako inaorodheshwa kati ya sherehe kuu.

Tukio hilo halisimuliwi na Biblia ya Kikristo, ila na Injili ya Yakobo, sura 1-5.

Kwa vyovyote, mama wa Yesu alizaliwa kweli kutoka uzao wa Abrahamu na taifa la Israeli katika karne ya 1 KK.

Tukio hilo liliandaa kabisa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kuwa Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndiye anayesadikiwa kuwa mzazi wa Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu ili kukomboa binadamu wote kutoka utumwa wa dhambi uliowapata tangu mwanzo kabisa[2].

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 311-312
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 266-268
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 70
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuzaliwa kwa Bikira Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.