Nenda kwa yaliyomo

Bikira Maria Malkia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa karne ya 6 mjini Roma: Santa Maria Regina (Mtakatifu Maria Malkia), ulio wa zamani kuliko yote inayojulikana.
Mchoro wa Giacomo di Mino, 13401350.

Bikira Maria Malkia ni kumbukumbu ya kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini inayolenga kumheshimu Bikira Maria kwa sababu alimzaa anayesadikiwa kuwa Mwana wa Mungu, mfalme wa amani, ambaye utawala wake hautakuwa na mwisho, hivyo Wakristo wanamsalimu kama Malkia wa mbingu na mama wa huruma[1].

Historia[hariri | hariri chanzo]

Adhimisho hilo lilianzishwa na Papa Pius XII mwaka 1955 na kupangwa tarehe 31 Mei, mwishoni mwa mwezi huo ambao sehemu mbalimbali unatumiwa na Wakatoliki kumheshimu Bikira Maria.

Lengo lake lilikuwa kutangaza kwamba, karibu na Kristo Mfalme wa ulimwengu, husimama mama yake, Bikira Maria, kama ilivyokuwa huko msalabani.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano tarehe ilibadilishwa na kuwa 22 Agosti, siku ya nane baada ya Maria kupalizwa mbinguni (15 Agosti)[2], kwa kuwa ndiyo utimilifu wa utukufu wa Maria mbinguni karibu na Mwanae.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria Malkia kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.