Yohakimu

From Wikipedia
Jump to navigation Jump to search
Watakatifu Yoakimu na Ana, wazazi wa Bikira Maria.

Yohakimu (kutoka Kiebrania יְהוֹיָקִים, Yəhôyāqîm, kwa Kigiriki Ἰωακείμ, Iōākeím, yaani "Yule ambaye YHWH amemuinua") anaheshimiwa kama baba wa Bikira Maria na babu wa Yesu kadiri ya mapokeo ya Ukristo na Uislamu, ingawa hatajwi katika Biblia[1] isipokuwa katika kitabu cha karne ya 2 kinachoitwa Injili ya Yakobo na vingine vilivyofuata.

Humo anatajwa pia mke wake Ana.

Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, hasa tarehe 26 Julai.

Katika Kurani anajulikana kama nabii Imran.

Tazama pia[edit | edit source]

Tanbihi[edit | edit source]

  1. Ronald Brownrigg, Canon Brownrigg Who's Who in the New Testament 2001 ISBN 0-415-26036-1 page T-62

Viungo vya nje[edit | edit source]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: