Ave Regina caelorum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muziki wa utenzi huo.

"Ave Regina Caelorum" (maana yake: 'Salamu Malkia wa Mbingu') ni utenzi wa Kikristo unaotumika katika liturujia ya Kanisa la Kilatini hasa kama antifona mojawapo ya kumalizia Sala ya mwisho nje ya Kipindi cha Pasaka</ref>[1][2][3].

Utenzi huo ulitungwa na mtu asiyejulikana katika karne ya 12 au kabla yake.

Maneno asili kwa Kilatini[hariri | hariri chanzo]

Ave, Regina caelorum,
Ave, Domina Angelorum:
Salve, radix, salve, porta
Ex qua mundo lux est orta:

Gaude, Virgo gloriosa,
Super omnes speciosa,
Vale, o valde decora,
Et pro nobis Christum exora.

Tafsiri huru ya Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

Salamu Malkia wa mbingu,
Malkia usiye kifani,
Malaika wanakuheshimu;
Salamu ewe Shina la Yese,
Salamu wewe Lango la Nuru,
Uliifungukia dunia,
Ili siku mpya ianze.

Ebu furahi, Ee Bikira,
Hakuna wa kukuzidi wewe,
Hata ukombozi wetu sisi
Ulianzishwa ndani mwako,
Sote watoto wako wapenzi
Utuombee kwa Kristo
Mkombozi wetu na Mwanao.[4]

Muziki wake[hariri | hariri chanzo]

Utenzi huo ulipambwa kwa muziki na watunzi mbalimbali.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]