Papa Pius V

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Pius V alivyochorwa na El Greco.

Papa Pius V, O.P. (17 Januari 15041 Mei 1572) alikuwa Papa kuanzia tarehe 7/17 Januari 1566 hadi kifo chake[1]. Alitokea Alessandria, Italia[2].

Alimfuata Papa Pius IV akafuatwa na Papa Gregori XIII.

Umuhimu wake katika historia ya Kanisa ni kwamba ndiye alishughulikia kwa moyo wa ibada na bidii ya kitume utekelezaji wa Mtaguso wa Trento kwa ajili ya urekebisho wa Kikatoliki, ukiwa pamoja na vitabu vya liturujia, katekesi na maadili, ili kueneza imani.

Anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Aprili[3].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Antonio Ghislieri.

Baadaye alijiunga na shirika la Wahubiri.

Kama kardinali, Ghislieri alijulikana kwa kutanguliza usahihi wa imani kuliko vyeo vya watu, akihukumu maaskofu wanane wa Ufaransa kwa uzushi. Vilevile alipinga upendeleo wowote kwa ndugu wa ukoo, akimkemea mtangulizi wake Papa Pius IV alipotaka kumfanya kardinali mtoto wa miaka 13 kwa kuwa ni ndugu yake, tena alipotaka kumsaidia ndugu mwingine kwa fedha za hazina ya Papa.

Kwa hati "Regnans in Excelsis" ya mwaka 1570, Pius V alitenga na Kanisa Katoliki malkia Elizabeth I wa Uingereza kwa uzushi na kwa kudhulumu Wakatoliki wa nchi yake.

Mwaka 1571 aliunganisha nchi za Kikatoliki katika "Liga Sancta" ambayo katika mapigano ya Lepanto, ingawa ilizidiwa na Dola la Osmani kwa idadi ya wanajeshi, ilifaulu kulizuia lisiteke Ulaya nzima. Pius V aliona ushindi huo umetokana na maombezi ya Bikira Maria aliyekuwa ameombwa sana kwa rozari siku zile, akaanzisha sikukuu ya Bibi Yetu wa Ushindi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Pius V kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.