Papa Yohane XII
Mandhari
Papa Yohane XII (takriban 937 – 14 Mei 964) alikuwa Papa kuanzia tarehe 16 Desemba 955 hadi kifo chake[1]. Alitokea Lazio, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Octavian[3], akiwa mzao wa Karolo Mkuu, vizazi saba kutoka kwake.
Alikuwa akihusiana na ukoo wa Tusculum na mwanachama wa familia mashuhuri ya Teofilatto ambayo ilikuwa imesimamia siasa za Mapapa kwa zaidi ya nusu karne. Upapa wake ukawa mbaya kwa madai ya udhalimu na maadili mabovu.
Alimfuata Papa Agapeto II akafuatwa na Papa Benedikto V.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Yohane XII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |