Papa Yohane XXIII
Papa Yohane XXIII (25 Novemba 1881 – 3 Juni 1963) alikuwa Papa kuanzia tarehe 28 Oktoba/4 Novemba 1958 hadi kifo chake[1]. Alitokea Sotto il Monte, Bergamo, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Angelo Giuseppe Roncalli. Watu walipenda kumuita "Papa mwema" kutokana na tabia yake ya kuvutia.
Alimfuata Papa Pius XII akafuatwa na Papa Paulo VI.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 3 Septemba 2000, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.
Mtu mwenye utu usio wa kawaida, kwa maisha, kazi na ari yake kubwa ya kichungaji alijitahidi kueneza kwa watu wote wingi wa upendo wake wa Kikristo na kuhamasisha umoja wa kidugu kati ya mataifa[3].
Umuhimu wa Papa huyu ni hasa kwamba aliitisha Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965) ambao ulikutanisha karibu maaskofu wote wa Kanisa Katoliki (wakati huo 3,000 hivi) na kuleta matengenezo mbalimbali ndani ya Kanisa hilo ili utume wake duniani kote ufanikiwe kama alivyotamani.
Ndiyo sababu sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba[4], siku aliyofungua mtaguso mkuu huo.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Angelo Giuseppe Roncalli alikuwa mtoto wa nne kati ya 14 wa familia ya mkoa wa Lombardia.[5] Alipata upadrisho tarehe 10 Agosti 1904 akapangwa sehemu mbalimbali, hata kama balozi wa Papa nchini Ufaransa, Bulgaria, Ugiriki na Uturuki.
Tarehe 12 Januari 1953 Papa Pius XII alimfanya Roncalli kuwa kardinali pamoja na kuwa Patriarki wa Venice.
Roncalli alichaguliwa kuwa Papa tarehe 28 Oktoba 1958 akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kura kupigwa mara 11 na tofauti na matarajio.
Papa Yohane XXIII alizidi kushangaza wote alipoitisha mtaguso mkuu pamoja na Sinodi ya Roma na urekebisho wa Mkusanyo wa Sheria za Kanisa tarehe 25 Januari 1959.
Yohane alifariki kwa kansa ya tumbo, miezi miwili baada ya kutoa barua yake maarufu Pacem in Terris kuhusu amani duniani.
Heshima baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Alizikwa katika mahandaki ya Basilika la Mt. Petro tarehe 6 Juni 1963 na kesi ya kumtangaza mtakatifu ilifunguliwa tarehe 18 Novemba 1965 na mwandamizi wake Papa Paulo VI. Baada ya kukubaliwa heshima kama Venerable tarehe 20 Desemba 1999, alitangazwa mwenye heri tarehe 3 Septemba 2000 pamoja na Papa Pius IX na watatu wengine.
Baada ya hatua hiyo, masalia yalisogezwa kwenye altare ya Mt. Jeromu yaweze kuonekana na waamini kwa urahisi.
Tarehe 5 Julai 2013, Papa Fransisko alisamehe uthibitisho wa muujiza wa pili aweze kutangazwa mtakatifu pamoja na Papa Yohane Paulo II tarehe 27 April 2014.[6][7]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/55725
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ "Pope John XXIII". IT: Vatican. Iliwekwa mnamo 2013-06-23.
- ↑ "Popes John Paul II, John XXIII to be declared saints in April", World News, Fox, Sep 30, 2013
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Antonimuthu, Rajamanickam (27 Aprili 2014). "Pope Francis declares Popes John Paul II and John XXIII Saints" (YouTube). Iliwekwa mnamo 27 Aprili 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]- Roncalli, Angelo Giuseppe (1965), Giovanni XXIII Il Giornale dell' Anima, White, Dorothy trans, Geoffrey Chapman, ISBN 0-225-66895-5
{{citation}}
: Unknown parameter|trans_title=
ignored (|trans-title=
suggested) (help). - Maandishi yake yote katika lugha mbalimbali
- Roncalli (Papa Yohane XXIII), Angelo Giuseppe, Opera Omnia (kwa Latin na Multilingual), EU: Documenta catholica omnia
{{citation}}
: Unknown parameter|trans_title=
ignored (|trans-title=
suggested) (help)CS1 maint: unrecognized language (link).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Hebblethwaite, Peter; Hebblethwaite, Margaret (2000). John XXIII: Pope of the Council. Continuum International. ISBN 0-8264-4995-6.
{{cite book}}
: Unknown parameter|lastauthoramp=
ignored (|name-list-style=
suggested) (help) - Martin, Malachi (1972), Three Popes and the Cardinal: The Church of Pius, John and Paul in its Encounter with Human History', Farrar, Straus & Giroux, ISBN 0-374-27675-7.
- ——— (1986). Vatican: a novel. New York: Harper & Row. ISBN 0-06-015478-0.
- ——— (1990). The Keys of this Blood. New York: Simon & Schuster. ISBN 0-671-69174-0.
- Williams, Paul L. (2003). The Vatican Exposed. Amherst, NY: Prometheus Books. ISBN 1-59102-065-4.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Yohane XXIII katika tovuti ya Vatikano
- Rockwell, Lew, John XXIII was embalmed; Vatican denies he is subject of miracle of incorruptibility.
- Wojtyła, Karol Józef (Sep 3, 2000), Pope John XXIII beatification mass (homily), Rome, IT: Vatican
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link). - "John XXIII", Pope John XXIII (biography), Rome, IT: Vatican.
- "John XXIII", Everything2.
- "Pope John XXIII", Atheism (biography), About, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-14, iliwekwa mnamo 2014-04-27
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - "John XXIII (pope)", Britannica (encyclopedia) (tol. la online).
- Advocating John XXIII as Righteous Among the Nations, Raoul Wallenberg.
- "John XXIII", Monuments, St Peter’s basilica.
- John XXIII (memorial), Find a grave.
- Pope John XXIII, Intra text: text with concordances and frequency list.
- "Saint of the Day", American Catholic, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-04-17, iliwekwa mnamo 2014-04-27
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - Pope John XXIII (news archive), UK: Pathé, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-04, iliwekwa mnamo 2014-04-27
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - "Pope John XXIII", Time (magazine), 4 Jan 1963, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-08-26, iliwekwa mnamo 2014-04-27
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link).
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Yohane XXIII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |