Papa Hilarius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Hilarius.

Papa Hilarius alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Novemba 461 hadi kifo chake tarehe 29 Februari 468[1]. Alitokea Sardinia, Italia[2].

Alimfuata Papa Leo I akafuatwa na Papa Simplicio.

Chini ya Papa Leo I alikuwa shemasi mkuu na alipigania haki za Kanisa. Pia alitumwa naye kama balozi kwenye Mtaguso wa pili wa Efeso (449) alipopata matatizo makubwa [3] kwa kumtetea Flaviano wa Kostantinopoli[4].

Baada ya kuchaguliwa aliendeleza sera za Papa Leo I kuhusu mamlaka ya Kanisa la Roma [5] na alipambana na makundi yaliyofarakana naye[3].

Aliandika barua muhimu kuhusu imani Katoliki ili kuthibitisha mitaguso mikuu ya Nisea, Efeso na Kalsedonia akiimarisha pia mamlaka ya Papa wa Roma kwa kuonyesha nafasi yake ya kwanza katika Kanisa lote.

Hatimaye anasifiwa kwa ujenzi wa makanisa mbalimbali mjini Roma.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 29 Februari (28 Februari katika miaka mifupi)[6], lakini pia 17 Novemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. ""Hilarius", Pontiffs, The Holy See".
  3. 3.0 3.1  One or more of the preceding sentences incorporates text from a publication now in the public domainKirsch, Johann Peter (1910). "Pope Saint Hilarus". In Herbermann, Charles. Catholic Encyclopedia. 7. Robert Appleton Company. http://www.newadvent.org/cathen/07348b.htm.
  4. Chapman, John. "Dioscurus." The Catholic Encyclopedia Vol. 5. New York: Robert Appleton Company, 1909. 31 March 2019
  5. ""Pope Hilarius". New Catholic Dictionary. CatholicSaints.Info. 11 May 2016".
  6. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Hilarius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.