Papa Anastasio I
Mandhari
(Elekezwa kutoka Papa Anastasius I)
Papa Anastasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 27 Novemba 399 hadi kifo chake tarehe 19 Desemba 401[1]. Alitokea Roma, Italia. Baba yake aliitwa Maximus.
Alimfuata Papa Siricius akafuatwa na mwanae aliyemzaa kabla hajapadrishwa, Papa Inosenti I, jambo la pekee katika historia ya Kanisa[2].
Mwenye ari kubwa, alilaani mafundisho kadhaa ya Origen na kuhimiza Wakristo wa Afrika Kaskazini wapinge Udonato[3].
Alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo, Jeromu na Paulino wa Nola. Jeromu alimsifu kama mtu mwenye utakatifu mkubwa na tajiri sana katika ufukara wake[4].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Desemba[5].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
- Mababu wa Kanisa
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]- Maandishi yake yote katika Patrologia Latina iliyotolewa na Migne.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ "Sant' Innocenzo I su santiebeati.it".
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/82250
- ↑ Campbell, Thomas (1907). "Pope St. Anastasius I". Catholic Encyclopedia. 1. New York: Robert Appleton Company.
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Anastasio I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |