Papa Siricius
Mandhari
Papa Siricius alikuwa Papa kuanzia tarehe 15 au 22 au 29 Desemba 384 hadi kifo chake tarehe 26 Novemba 399[1]. Alitokea Roma, Italia na baba yake aliiitwa Tiburtius.
Alimfuata Papa Damaso I[2] akafuatwa na Papa Anastasius I.
Alikuwa mtendaji na kukabili masuala mbalimbali. Amri zake 15 (hati Directa) kuhusu maisha ya Kanisa ni za kwanza kutufikia nzima bila kasoro.
Ambrosi alimsifu kama mwalimu halisi kwa sababu, akibeba mzigo wa wale wote wenye majukumu ya kiaskofu, aliwaelimisha kuhusu mafundisho ya mababu wa Kanisa, aliyoyathibitisha kwa mamlaka yake ya Kipapa pia[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
- Mababu wa Kanisa
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ ""The 38th Pope", Spirituality for Today, Diocese of Bridgeport". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-30. Iliwekwa mnamo 2022-04-10.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/90423
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Siricius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |