Nenda kwa yaliyomo

Papa Gregori III

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Gregori III.

Papa Gregori III alikuwa Papa kuanzia tarehe 18 Machi 731 hadi kifo chake tarehe 28 Novemba 741[1].

Alizaliwa katika nchi ya Syria[2], akiwa Papa wa mwisho kutokea nje ya Ulaya hadi alipochaguliwa Papa Fransisko mwaka 2013[3]. Baba yake aliitwa Yohane[4].

Alimfuata Papa Gregori II akafuatwa na Papa Zakaria.

Mara baada ya kuchaguliwa na umati wa waumini [5] na kuthibitishwa na mwakilishi wa kaisari wa Dola la Roma Mashariki[6] alimsihi Kaisari Leo III alegeze msimamo wake wa kupinga matumizi ya picha takatifu. Kwa kuwa balozi wake alikamatwa, Papa aliitisha Sinodi ya Roma (731) iliyolaani vikali msimamo huo[7], akapamba makanisa ya jiji lake kwa picha hizo.

Pamoja na maamuzi mengine, Papa Gregori III alisaidia uinjilishaji wa Wajerumani kwa kumfanya mmisionari Bonifas kuwa askofu mkuu na balozi wake huko Ujerumani[8]. Vilevile aliunga mkono kazi ya Wilibaldi hukohuko [9]

Alipaswa pia kupambana na uvamizi wa Walombardi katika Italia ya Kati akitegemea kwanza msaada wa kaisari, halafu ule wa Wafaranki, ambao hata hivyo hawakuitikia sana.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 10 Desemba[10].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. "Brusher S.J., Joseph. "St. Gregory III", Popes Through the Ages". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-21. Iliwekwa mnamo 2022-04-15.
  4. "The Cardinals of the Holy Roman Church". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2013. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Mann, p. 204
  6. Levillain, p. 643
  7. Treadgold, p. 354; Mann, p. 205
  8. Levillain, p. 644
  9. Mershman, Francis. "Sts. Willibald and Winnebald." The Catholic Encyclopedia Vol. 15. New York: Robert Appleton Company, 1912. 18 September 2017
  10. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Gregori III kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.