Papa Benedikto IX

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Papa Benedikto IX.

Papa Benedikto IX (takriban 1012 – baada ya 1055) alipata kuwa papa mara tatu: ya kwanza tangu Oktoba 1032 hadi Septemba 1044, ya pili tangu Aprili hadi Mei 1045, na ya tatu tangu Novemba 1047 hadi Julai 1048. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Theophylactus wa Tusculum.

Alimfuata mara ya kwanza Papa Yohane XIX, ya pili Papa Silvester III, na ya tatu Papa Klementi II.

Kila mara alifukuzwa madarakani kwa sababu ya matendo yake maovu au aliuza cheo chake.

Hatimaye alifuatwa na Papa Damaso II.

Mwaka wake wa kufariki haujulikani kwa uhakika. Mapokeo mbalimbali yanataja mwaka 1055, 1065 au 1085.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Pope.svg Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Benedikto IX kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.