Papa Nikolasi I
Papa Nikolasi I au Nikolasi Mkuu (takriban 820 – 13 Novemba 867) alikuwa Papa kuanzia tarehe 24 Aprili 858 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].
Alimfuata Papa Benedikto III akafuatwa na Papa Adriano II.
Anakumbukwa kwa kuimarisha mamlaka ya Papa wa Roma, akichangia ustawi wa cheo hicho, hasa katika Ulaya Magharibi. Alisisitiza kuwa mamlaka hiyo iko juu ya watawala pia katika masuala ya imani na maadili.
Alikataa kutangaza ubatili wa ndoa ya mfalme Lothari II wa Lotharingia na mke wake, ingawa mfalme aliudai ili kumuoa Waldrada, mtaguso fulani uliukubali na jeshi la Wafaranki lilizingira Roma.
Mahusiano na Dola la Roma Mashariki yaliharibika kwa sababu aliunga mkono Patriarki Ignasi wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa madarakani ili kumpisha Fosyo.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 13 Novemba[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Mapapa
Maandishi
[hariri | hariri chanzo]- Opera Omnia katika Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo=
[hariri | hariri chanzo]- Dvornik, Francis (1948). The Photian Schism: History and Legend. Cambridge, UK: Cambridge University Press.
- Gallagher, Clarence (2019). Church Law and Church Order in Rome and Byzantium: A Comparative Study. Taylor & Francis.
- Ostrogorsky, George (1956). History of the Byzantine State. Oxford: Basil Blackwell.
- Siecienski, Anthony Edward (2010). The Filioque: History of a Doctrinal Controversy. Oxford University Press. ISBN 9780195372045.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Nikolasi I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |