Ignasi wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Ignasi katika ukuta wa Hagia Sofia, Istanbul.

Ignasi wa Konstantinopoli (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 798 hivi – Konstantinopoli, 23 Oktoba 877) alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli miaka 847-858 halafu 867-877[1].

Farakano la muda la miaka 863-867 kati ya Kanisa la Roma na lile la Konstantinopoli kuhusu upatriarki wake na ule wa mshindani wake, Fosyo, lilikuwa baya kuliko yote kabla ya farakano la mwaka 1054 ambalo limedumu hadi leo kati ya Ukristo wa Magharibi na Waorthodoksi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu; alitangazwa rasmi na Fosyo mwenyewe mwaka 878.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.