Papa Agapeto I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Papa Agapetus I)
Jump to navigation Jump to search
Mt. Agapeto I

Papa Agapeto I alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Mei 535 hadi kifo chake tarehe 22 Aprili 536[1]. Alitokea Roma, Italia[2].

Alimfuata Papa Yohane II akafuatwa na Papa Silverio.

Alisimama imara dhidi ya Waario, pia alimwondoa madarakani Anthimus I, askofu mkuu wa Trabzon (Uturuki) aliyehamishimiwa na serikali kuwa Patriarki wa Konstantinopoli, kutokana na mafunzo yake yaliyoangaliwa na Kanisa Katoliki kuwa ya uzushi. Badala yake alimweka wakfu Mena wa Konstantinopoli.

Zimetufikia barua zake nne [3]

Muda si mrefu baada ya kifo chake alianza kuheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Pope.svg Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Agapeto I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.