Nenda kwa yaliyomo

Papa Agapeto I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Agapeto I

Mt. Agapeto I
Feast

Papa Agapeto I alikuwa Papa kuanzia tarehe 13 Mei 535 hadi kifo chake tarehe 22 Aprili 536[1]. Alitokea Roma, Italia[2].

Alimfuata Papa Yohane II akafuatwa na Papa Silverio.

Alidai kwa nguvu Papa achaguliwe na waklero wa Roma bila kuingiliwa na yeyote na hadhi ya Kanisa iheshimiwe popote pale.

Mfalme wa Wagoti Teodoto alimtuma Konstantinopoli kwa kaisari Justiniani I, na huko alisimama imara dhidi ya Waario, pia alimwondoa madarakani Anthimus I, askofu mkuu wa Trabzon (Uturuki) aliyehamishimiwa na serikali kuwa Patriarki wa Konstantinopoli, kutokana na mafunzo yake yaliyoangaliwa na Kanisa Katoliki kuwa ya uzushi. Badala yake alimweka wakfu Mena wa Konstantinopoli akafariki huko.

Zimetufikia barua zake nne [3]

Muda si mrefu baada ya kifo chake alianza kuheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Dudden, Frederick H. (1905), Gregory the Great, London: Longmans, Green, and Co
  • Louise Ropes Loomis, The Book of Popes (Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN 1-889758-86-8 (Reprint of the 1916 edition. English translation with scholarly footnotes, and illustrations).
  • Martindale, John R.; Jones, A.H.M.; Morris, John (1992), The Prosopography of the Later Roman Empire, Volume III: AD 527–641, Cambridge University Press, ISBN 978-0521201608 {{citation}}: Check |isbn= value: checksum (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Agapeto I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.