Papa Gelasio I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Papa Gelasius I)
Mt. Gelasius I.

Papa Gelasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 1 Machi 492 hadi kifo chake tarehe 21 Novemba 496[1]. Alikuwa Papa wa tatu mwenye asili ya Afrika kaskazini.[2][3][4]

Alimfuata Papa Felix III akafuatwa na Papa Anastasio II.

Alidai utiifu kwake kutoka kwa Wakristo wa Magharibi na Mashariki vilevile na kutetea kwa nguvu imani sahihi hata kuchangia mabishano, ingawa alikuwa na mahusiano mazuri na watawala Waostrogoti waliokuwa Waario[5].

Mwandishi mahiri[6], kati ya Mapapa wa karne za kwanza, ndiye aliyeandika zaidi. Mwaka 494, aliandika barua Duo sunt kwa kaisari Anastasius I kuhusu mahusiano ya Kanisa na Dola; barua hiyo aliathiri siasa kwa karibu miaka elfu.[7] Pia zimetufikia barua zake nyingine zaidi ya 100[8]. Maandishi mengine yalitajwa kuwa ya kwake ingawa si kweli; lengo lilikuwa kuyatia maanani zaidi.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 21 Novemba[9].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. Browne, M. (1998). "The Three African Popes.". The Western Journal of Black Studies 22 (1): 57–58. Retrieved 2008-04-10. 
  3. J.Conant, Staying Roman: Conquest and Identity in Africa and the Mediterranean, 439–700, CUP, 2012, p. 83.
  4. Book of Saints – Pope Gelasius (en-US) (2013-06-23).
  5. Cohen, Samuel (2022). "Gelasius and the Ostrogoths: jurisdiction and religious community in late fifth‐century Italy". Early Medieval Europe (in English) 30 (1): 22–23. ISSN 0963-9462. doi:10.1111/emed.12519. 
  6. The title of his biography by Walter Ullmann expresses this:Gelasius I. (492–496): Das Papsttum an der Wende der Spätantike zum Mittelalter (Stuttgart) 1981.
  7. Internet History Sourcebooks Project.
  8. Gelasius I (2014). Neil, Bronwen; Allen, Pauline, eds. The letters of Gelasius I (492-496) : pastor and micro-manager of the Church of Rome. Turnhout, Belgium. pp. 8–9. ISBN 978-2-503-55299-6. OCLC 893407493. 
  9. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Maisha yaliyoandikwa na Dionysius Exiguus, mwanafunzi wa Cassiodorus.
  • Norman F. Cantor, Civilization of the Middle Ages.
  • Cohen, Samuel (2022). "Gelasius and the Ostrogoths: jurisdiction and religious community in late fifth‐century Italy". Early Medieval Europe. 30 (1): 20–44. doi:10.1111/emed.12519. ISSN 0963-9462.
  • Neil, Bronwen, and Allen, Pauline (eds. and trans.). The letters of Gelasius I (492-496) : pastor and micro-manager of the Church of Rome. Turnhout, Belgium. pp. 8–9. ISBN 978-2-503-55299-6. OCLC 893407493.
  • Catholic Encyclopedia, 1908: [1]
  • Rudolf Schieffer, Gelasius I, in Lexikon des Mittelalters, Bd. 4 (1989), Sp. 1197.
  • Ullmann, W., Gelasius I. (492–496): Das Päpsttum an der Wende der Spätantike zum Mittelalter, Stuttgart, 1981.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Gelasio I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.