Papa Pius X

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Pius X.

Papa Pius X (2 Juni 183520 Agosti 1914) alikuwa Papa kuanzia 4 Agosti 1903 hadi kifo chake.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alitokea kijiji cha Riese, Veneto, Italia Kaskazini.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giuseppe Sarto.

Kabla ya kuchaguliwa kama Papa, aliwahi kuwa paroko, askofu wa Mantua(tangu 1884, halafu Patriarki askofu mkuu wa Venice (tangu 1893). Hivyo alikuwa na mang'amuzi mengi ya uchungaji|kichungaji.

Alimfuata Papa Leo XIII na kuvishwa taji tarehe 9 Agosti 1903, wa kwanza katika karne ya 20. Akafuatwa na Papa Benedikto XV.

Kwa kuwa katika uchaguzi ma[[kardinali walimpiga kura kwanza mwenzao Rampolla, lakini aliwekewa kura ya turufu na Kaisari wa Austria-Hungaria, mara alipochaguliwa Pius X alifuta haki hiyo ya Kaisari na kuamua atengwe na Kanisa Katoliki yeyote atakayeingilia tena uchaguzi wa Papa.

Lengo lake lilifafanuliwa na kaulimbiu yake: "Instaurare omnia in Christo" Kukamilisha yote ndani ya Kristo.

Kweli alijitahidi kuleta hali mpya katika Kanisa

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Pope.svg Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Pius X kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.