Nguvu (adili)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maadili bawaba
La Fortezza. Nguvu katika mchoro wa Sandro Botticelli, Firenze.

Nguvu (kwa Kigiriki ἀνδρεία - andreia; kwa Kilatini fortitudo) ni adili la kiutu linalomfanya mtu awe imara na kudumu kulenga mema hata katika matatizo.

Linathibitisha nia ya kushinda vishawishi na kushinda mapingamizi katika njia ya uadilifu. Linawezesha kushinda hofu hata ya kifo na kuvumilia majaribu na dhuluma. Hivyo mtu anakuwa tayari kuuawa ili kutetea jambo la haki.

Kuanzia Plato nguvu inatajwa kati ya maadili manne yanayoitwa maadili bawaba kwa kuwa yanategemeza maadili mengine yote ya kiutu.