Nenda kwa yaliyomo

Mfiadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mfiadini ni binadamu yeyote aliyeuawa kwa ajili ya imani au maadili ya dini aliyoiamini.

Inasikitisha kwamba katika historia dhuluma nyingi zilifanywa na serikali, viongozi na wafuasi wa dini na madhehebu tofauti, na watu wengine.

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya wataalamu wanakadiria Wakristo 70,000,000 waliuawa, wengi wao katika karne ya 20 chini ya sera za ukanamungu wa ukomunisti wa Urusi na nchi nyingine. Kati yao wanaongoza kwa wingi Waorthodoksi wakifuatwa na Wakatoliki.

Tangu alipouawa Stefano, wa kwanza kati yao, waamini waliheshimu watu wa namna hiyo kwa namna ya pekee wakiona wametekeleza hasa upendo mkuu nyuma ya Yesu msulubiwa.

Kwa mfano wake mtu wa namna hiyo aliitwa shahidi (kwa Kigiriki μάρτυς, martyur).