Nenda kwa yaliyomo

Stefano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Stefano alivyochorwa na Giotto.

Stefano (aliuawa Yerusalemu, Israeli/Palestina, 36 hivi BK) ni mfiadini wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo.

Habari zake zinapatikana katika kitabu cha Matendo ya Mitume kuanzia sura ya 6.

Myahudi mwenye kutumia zaidi lugha ya Kigiriki, ni wa kwanza kati ya wanaume 7 waliowekewa mikono na Mitume wa Yesu kwa ajili ya kutoa huduma.

Mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, kutokana na juhudi zake, alikabiliana na chuki ya Wayahudi wenye msimamo mkali, akawa wa kwanza kati ya wafuasi wa Yesu kumwaga damu yake mwenyewe kwa kumtolea ushahidi wa imani kama Kristo, akisema anamuona katika utukufu ameketi kuume kwa Baba [1].

Katika kufa alizidi kumuiga Yesu kwa kuwaombea msamaha watesi wake akamkabidhi roho yake. Maneno yake ya mwisho yalikuwa haya: "Bwana Yesu, pokea roho yangu… Bwana, usiwahesabie dhambi hii." (Mdo 7:59-60)

Mhusika mkuu wa kifodini chake alikuwa Farisayo jina lake Saulo, maarufu zaidi baada ya uongofu wake kama Mtume Paulo.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu yote ya Ukristo yanayokubali hadhi hiyo.

Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu yake tarehe 26 Desemba[2], mara baada ya Noeli, wakati Waorthodoksi wanafanya hivyo tarehe 3 Agosti.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stefano kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.