Maadili bawaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maadili bawaba

Maadili bawaba ni maadili manne ya kiutu yaliyojulikana na wanafalsafa wa Ugiriki, hasa Plato na Aristotle, kuwa ndiyo yanayotegemeza maadili mengine yote ya kiutu, kama vile bawaba zinavyotegemeza mlango uweze kufanya kazi yake vizuri. Yanaitwa pia maadili ya kiutu ya msingi au fadhila za msingi, kwa kuwa ndiyo hasa yanayomfanya mtu atende kadiri ya utu wake.

Majina yake ni: busara, haki, nguvu na kiasi.

Katika Ukristo yanatofautishwa na maadili ya Kimungu, yaani imani, tumaini na upendo ambayo yanatokana na Mungu na kumlenga yeye.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]