Nenda kwa yaliyomo

Sufu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sufu ya kondoo wakati wa majira ya baridi
Sufu iliyokatwa na kusafishwa; kulia: uzi fupi; kushoto: uzi ndefu

Sufu (pia: sufi, tazama pale; kutoka kar. صوف suf[1]) ni nywele manyoya laini za wanyama mbalimbali kama vile kondoo, mbuzi, ngamia, lama au sungura zinazofaa kusokotwa kuwa uzi ndefu kwa matumizi ya nguo au matandiko na blanketi.

Sufu ilianza kutumiwa kwa nguo tangu miaka 4000 KK na watu wamechagua wanyama wanaofaa na kuwafuga kwa tabia hii. Leo hii kiasi kikubwa kabisa cha sufu kinapatikana kutokana na kondoo. Nchi ya Australia ina kondoo nyingi duniani inazaa asilimia 30 za mahitaji ya sufu duniani.


Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  1. neno asilia katika Kiarabu صوف suf lamaanisha nywele manyoya laini ya kondoo na wanyama wengine limeingia katika Kiswahili kwa maumbo ya sufi na sufu