Sufi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kwa mwelekeo wa kidini tazama Sufii, Usufii
Sufi katika tunda la mti aina ya Ceiba pentandra kisiwani Unguja
Mti wa msufi pori (Bombex Rhodognaphalon)

Sufi (kar. صوف suf[1]) ni jina kwa nyuzi laini kama pamba zinazotoka kwenye matunda ya msufi (miti ya aina za bombax na ceiba).

Sufi hutumiwa kwa kujaza magodoro n.k.. Hafai kwa kutengeneza nyuzi ndefu na kitambaa.

Mara nyingi neno hili latumiwa pia kwa kutaja sufu yaani manyoya ya kondoo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. neno asilia katika Kiarabu صوف suf lamaanisha nywele manyoya laini ya kondoo na wanyama wengine limeingia katika Kiswahili kwa maumbo ya sufi na sufu