Godoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Godoro la kisasa.

Godoro ni kifaa kikubwa cha kusaidia mwili kupumzika. Hutumiwa kama kitanda au kama sehemu ya kitanda. Godoro huwekwa kwenye chaga ya kitanda na kulaliwa.

Godoro huwa na kitambaa cha juu ambacho ndani yake huenda kukawa na sponji, nyasi, nywele au pamba. Godoro za kisasa huenda zikawa na maji au hata hewa iliyowekwa kwenye kifuko kisicho na vishimo na kitakachoweza kubeba yaliyomo ndani yake.

Historia ya godoro[hariri | hariri chanzo]

Godoro lilivumbuliwa na Waarabu na jina la Kiingereza Mattress lamaanisha 'kuweka chini' katika lugha ya Kiarabu.

Wakati wa vita vya msalaba, magodoro yalitumika kulalia chini. Tabia hii ilikuwa kuiga Waarabu waliokuwa wakilalia magodoro na hata mikeka iliyowekwa chini.

Magodoro haya ya hapo zamani yalijazwa nyasi, manyoya ya ndege au hata nywele za farasi.

Magodoro ya zamina kabisa yaliyoko kwa historia yaonekana kuwa na takribani miaka 77,000.

Magodoro ya kisasa[hariri | hariri chanzo]

Godoro za kisasa hujazwa kwa sponji au hata mpira (rubber) na hujulikana kama innerspring kwani huweza kupinda na kukunjika kwa urahisi. Haswa yale ya vitanda vya hospitali huwa ni innerspring, kwani vitanda vya hospitali hukunjwa ili mgonjwa apate kustareheka.

Magodoro ya kisasa huenda pia yakawa na uwezo wa kupashwa kawi ya umeme ili kuweka joto katika kitanda.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Godoro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.