Paroko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Paroko ni padri aliyekabidhiwa na Askofu uchungaji wa parokia.

Jina hilo linatokana na Kigiriki cha zamani πάροικος (pàroikos), ambapo asili ni kitenzi παρà οἰκεω (parà oikéo), yaani "kuishi jirani", "kuishi kandokando", kulingana na Askofu aliyeishi mbali, katika Kanisa kuu.

Katika Kanisa Katoliki la Kilatini huduma ya maparoko inaratibiwa na Mkusanyo wa Sheria za Kanisa katika kanuni 519-534.