Parokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Parokia ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa Kanisa Katoliki, ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya jimbo (dayosisi) unapofanyika uchungaji wa kila siku chini ya kasisi anayemwakilisha Askofu.

Kiini cha maisha ya parokia ni adhimisho la Ekaristi siku ya Jumapili, ambapo jumuia nzima ya Kikristo ya eneo husika inakusanyika isikilize Neno la Mungu, imsifu Mungu na Kumega mkate.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina hilo lilianza kutumika katika karne III kutokana na neno la Kigiriki παρоικια (=ujirani) linalotumika katika tafsiri ya Biblia ya Septuaginta kwa maana ya kukaa ugenini.

Katika Sheria za Kanisa Katoliki[hariri | hariri chanzo]

Kanuni 515 za Sheria za Kanisa la Kilatini inasema, "Parokia ni jumuia rasmi ya waamini ambayo imeundwa kwa namna ya kudumu ndani ya Kanisa maalumu na imekabidhiwa kichungaji kwa paroko kama mchungaji wake chini ya mamlaka ya Askofu wa jimbo. Ni juu ya Askofu wa jimbo tu kuanzisha, kufuta na kubadilisha parokia; lakini asizianzishe, asizifute wala asizibadilishe sana kabla hajapokea maoni ya Halmashauri ya mapadri. Parokia iliyoundwa kihalali papo hapo ina hadhi ya nafsi ya kisheria".

Katika madhehebu mengine[hariri | hariri chanzo]

Mbali ya Kanisa Katoliki, ambalo lina mtandao mkubwa zaidi wa parokia duniani kote, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na Wakristo wengine kadhaa wanatumia muundo wa namna hiyo, ingawa mikazo ni tofauti, kulingana na teolojia yao.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Parokia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.