Halmashauri ya mapadri
Halmashauri ya mapadri (kwa Kiingereza: Presbyteral Council au Council of Priests[1]) ni muundo muhimu wa majimbo yote ya Kanisa Katoliki.
Lengo lake ni kuhakikisha kwamba mapadri, kupitia wawakilishi wao, wanashiriki mamlaka ya askofu katika kuongoza jimbo lake.
Kwa Kanisa la Kilatini, kanuni 495 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa imeagiza halmashauri ya namna hiyo iwepo katika majimbo yote ili kukabili masuala ya kichungaji.
Kanuni 497 inadai kama nusu wawe wamechaguliwa na mapadri wote, na waliobaki washike nafasi kutokana na vyeo walivyonavyo au kwa kuteuliwa na askofu mwenyewe.
Ni yeye atakayeamua lini akutanishe washauri wake hao, atakayeendesha kikao na kupanga masuala ya kujadiliwa [2].
Jimbo likibaki bila askofu, halmashauri inakoma na majukumu yake yanatimizwa na Jopo la washauri.[3]
Sheria za namna hiyohiyo zimo katika kanuni 264 n.k. za Mkusanyo wa Kanuni za Makanisa ya Mashariki (kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Code of Canon Law, canons 495-501
- ↑ Canon 500 §1
- ↑ Canon 501 §2
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Halmashauri ya mapadri kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |