Jopo la washauri
Mandhari
Jopo la washauri katika sheria za Kanisa Katoliki lote (Kanisa la Kilatini na Makanisa Katoliki ya Mashariki vilevile) ni kundi la mapadri sita hadi kumi na wawili walioteuliwa na askofu wa jimbo kati ya wale wa halmashauri ya kichungaji ili wamsaidie kwa karibu katika masuala mbalimbali, hasa ya uchumi.
Jimbo likibaki bila askofu, ni juu ya jopo hilo kumchagua msimamizi wa kijimbo ambaye ashike kwa muda nafasi yake.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jopo la washauri kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |