Halmashauri ya kichungaji
Halmashari ya kichungaji ni muundo wa Kanisa Katoliki katika ngazi ya jimbo na ya parokia.
Lengo lake ni kuwezesha waumini wote (makleri, watawa na walei), kupitia wawakilishi wao, kufanya utafiti, kujadili na hatimaye kutoa mashauri kwa askofu au paroko kuhusu masuala ya uchungaji: umisionari, katekesi, malezi, sakramenti n.k.[1].
Mpango huo ulihimizwa mwaka 1965 na mtaguso wa pili wa Vatikano (hati Christus Dominus, 27).
Baadaye kanuni 511 ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa (kwa Kanisa la Kilatini) imesema kuhusu halmashauri ya kijimbo [2] na kanuni 536 kuhusu halmashauri ya kiparokia[3]
Hivyo, uamuzi wa kuanzisha halmashauri kiparokia unamtegemea askofu wa jimbo, baada ya kusikiliza halmashauri ya mapadri.
Sheria za namna hiyohiyo zimo katika Mkusanyo wa Kanuni za Makanisa ya Mashariki (kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Congregation for the Clergy (1973), Omnes Christifideles, www.pastoralcouncils.com
- ↑ "In each diocese, to the extent that pastoral circumstances recommend it, a pastoral council is to be established whose responsibility it is to investigate under the authority of the bishop all those things which pertain to pastoral works, to ponder them and to propose practical conclusions about them.""Chapter V. The Pastoral Council", Code of Canon Law, Libreria Editrice Vaticana
- ↑ "§1. If the diocesan bishop judges it opportune after he has heard the presbyteral council, a pastoral council is to be established in each parish, over which the pastor presides and in which the Christian faithful, together with those who share in pastoral care by virtue of their office in the parish, assist in fostering pastoral activity. §2. A pastoral council possesses a consultative vote only and is governed by the norms established by the diocesan bishop.""Chapter VI. Parishes, Pastors, and Parochial Vicars", Code of Canon Law, Libreria Editrice Vaticana
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Mark F. Fischer, Pastoral Councils in Today's Catholic Parish (Mystic, CT: Twenty-Third Publications - Bayard, 2001), ISBN 1-58595-168-4.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Parish Pastoral Councils, edited by Mark F. Fischer
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Halmashauri ya kichungaji kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |