Liturujia ya Milano
Liturujia ya Milano ni liturujia maalumu ambayo inatumika katika sehemu kubwa ya jimbo kuu la Milano na katika parokia kadhaa za majimbo ya kandokando (Lecco, Como, Bergamo, Novara na Lodi) nchini Italia hadi baadhi ya zile za jimbo la Lugano (Uswisi).
Kesi ya pekee ni parokia ya Pescocostanzo iliyopo katika Italia ya kati inapotumika kwa ibada ya ubatizo.
Kama asili yake anatajwa babu wa Kanisa Ambrosi, aliyekuwa askofu wa jimbo hilo katika sehemu ya mwisho wa karne ya 4. Ndiyo sababu inaitwa pia Liturujia ya Ambrosi.
Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano liturujia hiyo imeshughulikiwa sana na wachungaji na wataalamu mbalimbali hata kupata uhai mpya.
Ingawa Wakatoliki wa maeneo hayo (milioni 5 hivi) wanafuata liturujia hiyo, upande wa sheria za Kanisa hawatofautiani na wenzao wote wa Kanisa la Kilatini.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Dizionario di Liturgia Ambrosiana (tol. la Marco Navoni). Milan. 1996. ISBN 88-7023-219-0.
{{cite book}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) - Griffiths, Alan (1999). We Give You Thanks and Praise. Canterbury Press. ISBN 1-58051-069-8.
- A. Ratti / M. Magistretti, Missale Ambrosianum Duplex, Mediolani 1913
- Missale Ambrosianum iuxta ritum Sanctae Ecclesiae Mediolanensis, ex decreto Sacrosancto OEcumenici Concilii Vaticani II instauratum, auctoritate Ioannis Colombo Sanctae Romanae Ecclesiae Presbyter Cardinalis Archiepiscopi Mediolanensis promulgatum, Mediolani 1981
- Messale Ambrosiano secondo il rito della santa Chiese di Milano. Riformato a norma dei decreti del Concilio Vaticano II. Promulgato dal Signor Cardinale Giovanno Colombo, arcivescovo di Milano, Milano 1976
- Messale ambrosiano festivo. Piemme. 1986. ISBN 88-384-1421-1.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholic Encyclopedia article
- Ambrosian Rite resources Archived 22 Oktoba 2020 at the Wayback Machine.
- The Ambrosian Rite Archived 21 Novemba 2020 at the Wayback Machine. (Kiitalia)
- http://www.archive.org/details/ambrosianliturgy00cathuoft
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Milano kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |