Majadiliano:Parokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Parokia-madhehebu mengine?[hariri chanzo]

Jinsi ninavyoelewa "parokia" ni muundo wa kanisa katoliki kwa sababu inaangalia kitengo cha kimahali kanisani kama wajibu wa "paroko" au padre kiongozi anayemwakilisha askofu.

Katika mafundisho ya kiprotestanti askofu si muhimu hivi (au: kwa wengine hayupo kabisa). Kanisa lenyewe ni umoja au ushirika wa wakristo kwenye mahali fulani. Lakini tabia muhimu kwenye ngazi hii ni "ushirika" (yaani ushirikiano, umoja) wa wakristo wenyewe wanaounganishwa kwa nguvu ya roho mtakatifu. Swali la padre au mchungaji si jambo la msingi - ushirika ni ushirika hata pasipo na padre au mchungaji. Kutegemeana na utaratibu wa dhehebu inawezekana ya kwamba ibada fulani (ekaristia, chakula cha Bwana) zinapaswa kusibiri kuwepo kwa mtumishi aliyewekwa wakfu kwa huduma hii lakini bado ni ushirika.

Kwa hiyo nauliza je kuna Waluteri wanaotumia lugha ya "parokia" katika Tanzania? Kama wako naombe ielezwe ni wapi. Menginevyo ningeongeza maelezo ya kwamba mafundisho ya "parokia" ni tofauti na "ushirika" kwa hiyo waprotestanti wanaiona tofauti. --Kipala (majadiliano) 22:48, 9 Machi 2009 (UTC)[reply]

Nyongeza: makala inahitaji masahihisho jinsi nilivyoandika hapa juu. Sina uhakika ni madhehebu gani yanayotumia jina "parokia" kwa Kiswahili; "Parish" kwa Kiingereza hutumiwa pia na Waanglikana na Wapresbiteri na Wamethodisti. Ila tu theolojia ni tofauti yaani kama ni jumuiya ya wakristo chini ya padre/mchungaji fulani au jumuiya ya wakristo pamoja na mchungaji/wachungaji wao (kama wako). --Kipala (majadiliano) 23:14, 13 Machi 2009 (UTC)[reply]
Ndugu, nilifikiri mabadiliko niliyofanya tarehe 13 Machi yalilingana na ujumbe wako wa kwanza. Kumbe naona hujaridhika bado. Labda jaribu kurekebisha wewe ili wote turidhike. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:02, 16 Machi 2009 (UTC)[reply]