Paulino wa Nola

Mtakatifu Paulino wa Nola (jina kamili: Pontius Meropius Anicius Paulinus; takriban 355 – 22 Juni 431) alikuwa askofu wa Kanisa huko Nola, karibu na Napoli, Italia.
Tangu kale ametambuliwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 22 Juni[1].
Maisha[hariri | hariri chanzo]
Paulino wa Nola alizaliwa katika mji wa Bordeaux nchini Ufaransa mwaka 355 hivi.
Alikuwa mtu maarufu, akaoa na kupata mtoto wa kiume.
Lakini alitamani kuishi maisha maadilifu, na hivi akabatizwa, akaachana na mali yake yote, akaanza kuishi kimonaki huko Nola, katika mkoa wa Campania nchini Italia, kuanzia mwaka wa 393.
Aliteuliwa kuwa askofu wa Nola, ambako alikuza sana heshima kwa Mt. Felix wa Nola, na kuwasaidia waliokwenda huko kuhiji.
Vilevile alijitahidi kupunguza taabu za watu wa wakati huo.
Aliandikiana barua na watu wengi maarufu, kama vile Agostino wa Hippo, akatunga mashairi kadhaa yenye usanifu wa hali ya juu sana.
Alikufa tarehe 22 Juni, mwaka 431.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Mababu wa Kanisa
Maandishi[hariri | hariri chanzo]
- Ausonius, & Paulinus of Nola, Ausone et Paulin de Nole correspondance, tr. D. Amherdt (2004) [Latin text; French tr.]
- Paulinus of Nola, Sancti Pontii Meropii Paulini Nolani Opera, ed. G. de Hartel (2nd. ed. cur. M. Kamptner, 2 vols., 1999) [v.1. Epistulae; v.2. Carmina. Latin texts]
- Paulinus of Nola, Paolino di Nola I Carmi ..., ed. A. Ruggiero (1996)
- Paulinus of Nola, Paolino di Nola Le Lettere. Testo latino con introduzione, traduzione italiana ..., ed. G. Santaniello (2 vols., 1992)
- Paulinus of Nola, The Poems of Paulinus of Nola translated ... by P. G. Walsh (1975)
- Paulinus of Nola, Letters of St Paulinus of Nola translated ... by P. G. Walsh (2 vols., 1966-7)
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- C. Conybeare, Paulinus Noster Self and Symbols in the Letters of Paulinus of Nola (2000)
- Trout, Dennis E (1999). Paulinus of Nola - Life, Letters, and Poems. Berkeley: University of California Press. ISBN 978-0-520-21709-6.
- Gardner, Edmund G. (editor) (1911. Reprinted 2010). The Dialogues of Saint Gregory the Great. Merchantville, NJ: Evolution Publishing. -- Chapter III of the Dialogues contains a long anecdote about Paulinus.
- J. Morelli, De S. Paulini Nolani Doctrina Christologica (Theology Doctorate dissertation, Pontificia Facultas Theologica Neapolitana apud Majus Seminarium, ex Typographica Officina Forense, Neapoli, MCMXLV)
- J. T. Lienhard, "Paulinus of Nola and Early Western Monasticism, with a study of the Chronology of His Work and an Annotated Bibliography," 1879-1976 (Theophaneia 28) (Köln-Bonn 1977), pp. 192–204;
- C. Magazzù, 'Dieci anni di studi su Paolino di Nola' (1977–1987), in Bollettino di studi latini 18 (1988), pp. 84–103;
- C. Iannicelli, 'Rassegna di studi paoliniani' (1980–1997), in Impegno e Dialogo 11 (1994–1996) [pubblic.1997], pp. 279–321 Rassegna Iannicelli
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Sons of San Paolino
- East Harlem Giglio Society
- Hotuba ya Papa Benedikto XVI juu ya Paulinus
- Giglio USA Archived 3 Aprili 2005 at the Wayback Machine.
- (Kiitalia) San Paolino de Nola
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |