Napoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sehemu ya mji wa Napoli
Napoli

Lua error in Module:Location_map at line 510: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Italia" does not exist.Mahali pa Napoli katika Italia

Majiranukta: 40°50′00″N 14°15′00″E / 40.833333°N 14.25°E / 40.833333; 14.25
Nchi Italia
Mkoa Campania
Wilaya Napoli
Idadi ya wakazi
 - 963,357
Tovuti: http://www.comune.napoli.it/

Napoli (kwa Kiingereza: Naples) ni mji wa bandari kando ya bahari ya Mediteranea katika Italia ya kusini.

Idadi ya wakazi inakaribia milioni 1. Mwaka 2015 lilianzishwa jiji la Napoli lenye watu 3,114,053 katika eneo dogo lenye msongamano mkubwa (2672 wakazi kwa kilometa mraba).

Ni mji wa kale sana na jina la "Napoli" ni umbo la Kiitalia la "Neapolis" lililokuwa jina asilia la Kigiriki. Maana mji huu ulianzishwa na Wagiriki wa Kale mnamo karne ya 6 KK. Jina la Kigiriki lina maana ya "mji mpya".

Mji uko kando ya mlima wa volkeno wa Vesuvio. Wataalamu wengine wanaona hatari ya mlipuko wa volkeno wa karibuni unaoweza kuharibu mji na wakazi wake wengi.

Sehemu ya kati ya mji imo katika orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Italy looking like the flag.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Napoli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.