Yesu kutolewa hekaluni
Yesu kutolewa hekaluni ni tukio la utoto wake, siku arubaini baada ya kuzaliwa, iliyopangwa na Torati kuwa siku ya kumtakasa mama yeyote aliyemzaa mtoto wa kiume.
Siku hiyo aliletwa na Yosefu na Maria katika hekalu la Yerusalemu akiwa mtoto wa kiume wa kwanza akakombolewa kwa sadaka ya fukara. Ndipo alipotambuliwa na kutangazwa na wazee wawili watakatifu, Simeoni na Anna.
Katika Injili[hariri | hariri chanzo]
Habari hiyo inasimuliwa na Luka mwinjili tu kama ifuatavyo:
Lk 2:22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. 23 Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana." 24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana.
25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Masiha wa Bwana. 27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu na kusema: 29 "Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani. 30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako, 31 ambao umeutayarisha mbele ya watu wote: 32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli."
33 Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako."
36 Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. 37 Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana. 38 Saa hiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na akaeleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu.
39 Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya. 40 Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa pamoja naye.
Katika liturujia[hariri | hariri chanzo]
Tukio hilo linaadhimishwa na Wakristo wengi siku 40 baada ya Noeli.
Katika Ukristo wa magharibi sikukuu hiyo iliwahi kuitwa pia "Mweuo wa Bikira Maria"; siku yake ni tarehe 2 Februari.
Wanaosali Rozari wanalitumia tukio hilo kama fungu la nne kati ya mafumbo ya furaha.
Picha[hariri | hariri chanzo]
Kutolewa Hekaluni kadiri ya Ambrogio Lorenzetti, 1342 (Galleria degli Uffizi, Florence), Italia
Kristo Kutolewa Hekaluni katika Misale ya Sherbrooke
James Tissot, Yesu Kutolewa Helaluni, Brooklyn Museum, Marekani
Kioo cha rangi katika kanisa kuu la Mt. Mikaeli, Toronto, Kanada
Menologion ya Basili II (1000 hivi)
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Schiller, Gertud, Iconography of Christian Art, Vol. I, 1971 (English trans from German), Lund Humphries, London, ISBN 0-85331-270-2
- Food and Feast in Medieval England, P. W. Hammond, ISBN 0-7509-0992-7
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- "Candlemas" article from The Catholic Encyclopedia, F. G. Holweck
- Sketch of Egeria's record of her pilgrimage, with quoted passages Archived Februari 17, 2007 at the Wayback Machine.
- Egeria's description of the liturgical year at Jerusalem
- Text of Luke 2 in the New Revised Standard Version Archived Februari 20, 2007 at the Wayback Machine.
- Traditions: Celebrating Candlemas Archived Desemba 23, 2016 at the Wayback Machine.
- Origins of Candlemas Cantica Nova
- History of the feast of the Purification/Candlemas Archived Julai 16, 2011 at the Wayback Machine. Latin Mass Society
- Liturgical Resources—Candlemas
- The Meeting of Our Lord in the Temple Archived Februari 20, 2008 at the Wayback Machine. from the Prologue from Ochrid by St. Nikolai Velimirovich
- Poems by Robert Herrick including "Upon Candlemas Eve" Archived Februari 24, 2007 at the Wayback Machine.
|
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yesu kutolewa hekaluni kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |