Misale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Misale ya karne XII huko Modena (Italia).

Misale, katika Kanisa Katoliki la Magharibi, ni kitabu cha liturujia kinachokusanya yale yanayohitajika kuadhimishia Misa (matini ya sala na nyimbo, pamoja na taratibu za vitendo mbalimbali n.k.).

Missale plenum (yaani Misale kamili) ilitokea katika Kanisa la Kilatini kwenye karne XI ili kukusanya pamoja yaliyokuwemo katika vitabu mbalimbali vilivyohitajika kwa Misa: Sakramentari yenye sala, Injili, Kitabu cha masomo mengine kutoka Biblia, Graduale yenye nyimbo.

Missale plenum ilienea kote kati ya karne XIII na ile ya XV.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, masomo yaliondolewa katika Misale na kurudishwa katika vitabu tofauti vya kutumiwa kwenye mimbari, wakati Misale inatakiwa kutumika kwenye kiti cha padri na altareni.