Nenda kwa yaliyomo

Ana (nabii)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ana siku ya Yesu kutolewa hekaluni, mchoro wa Giotto, Padova, Italia.

Ana (kwa Kiebrania חַנָּה, Hannah, kwa Kigiriki Ἄννα, Anna) alikuwa mwanamke wa karne ya 1 KK katika Israeli.

Ni maarufu kama nabii kutokana na habari iliyomo katika Injili ya Luka (2:36-38[1]).

Humo tunaambiwa kwamba alikuwa binti Fanueli, wa kabila la Asheri.

Alipoachwa mjane ujanani baada ya miaka 7 ya ndoa, alihamia hekalu la Yerusalemu akifunga chakula na kusali hadi miaka 84.[2][3][4][5][6][7][8]

Mtoto Yesu alipoletwa hekaluni siku 40 tu baada ya kuzaliwa, Ana alitangaza habari zake kwa waliokuwepo.

Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu nabii.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3[9] au 16 Februari.[10][11]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
 1. 2:22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana. 23 Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana." 24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana. 25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Masiha wa Bwana. 27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu na kusema: 29 "Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa amani. 30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu utokao kwako, 31 ambao umeutayarisha mbele ya watu wote: 32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli." 33 Baba na mama yake Yesu walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, "Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako." 36 Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. 37 Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana. 38 Saa hiyohiyo alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na akaeleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu. 39 Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na Sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, mkoani Galilaya. 40 Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa pamoja naye.
 2. Cyclopædia of Biblical, theological, and ecclesiastical literature Vol 1 p.235. John McClintock,James Strong. Iliwekwa mnamo 2010-01-16.
 3. Easton's Dictionary
 4. The Greek text states that "she was a widow of eighty four years".UBS Greek NT καὶ αὐτὴ χήρα ὡς ἐτῶν ὀγδοηκοντατεσσάρων. The passage is ambiguous: it could mean that she was 84 years old, or that she had been a widow for 84 years.
 5. Twelve Extraordinary Women: How God Shaped Women of the Bible, and ... – Page 136 John MacArthur – 2008 "The Greek text is ambiguous as to her exact age. (“This woman was a widow of about eighty-four years.”) It might mean literally that she had been a widow for eighty-four years. Assuming she married very young (remember, thirteen was a ..."
 6. Green, Joel B., The Gospel of Luke, Eerdmans, 1997, ISBN 0-8028-2315-7, p. 151.
 7. Marshall, I. Howard, The Gospel of Luke: A commentary on the Greek text, Eerdmans, 1978, ISBN 0-8028-3512-0, p. 123.
 8. Elliott, J.K., "Anna's Age (Luke 2:36–37)," Novum Testamentum, Vol. 30, Fasc. 2 (Apr., 1988), pp. 100–102.
 9. Martyrologium Romanum
 10. "Afterfeast of the Meeting of our Lord in the Temple". Orthodox Church of America. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-30. Iliwekwa mnamo 2007-09-05. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
 11. February 3 is the feast day of the elder Simeon and the prophetess Anna Byzantine Catholic Archeparchy of Pittsburgh)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ana (nabii) kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.