Mwinjili Luka
Mwinjili Luka (kwa Kigiriki Λουκᾶς, Lukas) ni Mkristo wa karne ya 1 ambaye tangu zamani za Mababu wa Kanisa anasadikiwa kuwa mwandishi wa Injili ndefu kuliko zote za Biblia ya Kikristo. Humo alisimulia kwa ufasaha na kupanga kwa utaratibu mzuri matendo na mafundisho ya Yesu, akastahili kuitwa "mwandishi wa upole wa Kristo" (Dante Alighieri)[1].
Vilevile anasadikiwa kuwa mwandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume kinachoendeleza Injili hiyo ili kuonyesha kazi ya Yesu Kristo ilivyoendelea katika Kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu hadi mwaka 63 BK.
Hivyo Luka, mtunzi pekee wa Agano Jipya asiye Myahudi, anahesabiwa kuwa ameandika robo ya sehemu hiyo ya pili ya Biblia nzima ya Ukristo.
Pamoja na Wakristo wengine wengi, Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu na msimamizi wa madaktari hasa katika sikukuu yake, tarehe 18 Oktoba[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Luka alizaliwa katika familia ya Kiyunani, labda mjini Antiokia ya Syria, leo nchini Uturuki.
Inasadikiwa aliongozwa na Mtume Paulo kumpokea Yesu na alifanya naye kazi kwa takribani miaka 18. Pamoja na ukaribu huo, hata hivyo hakuandika tu mitazamo ya Paulo, hii ni kuonesha kuwa aliyaandika yale aliyovuviwa na Roho Mtakatifu baada ya utafiti wa kihistoria katika vyanzo mbalimbali.
Anatajwa na Paulo katika barua zake kama mganga aliye jirani naye katika majaribu yake: Waraka kwa Filemoni, mstari 24; Waraka kwa Wakolosai 4:14 na Waraka wa pili kwa Timotheo 4:11.
Uaminifu huo wa Luka kwa Paulo unalingana na habari za Matendo ya Mitume, ambapo Luka hajitaji, lakini anasimulia safari za Paulo akitumia mara nyingi neno "sisi". Hivyo anajishuhudia kuwa mshiriki wa utume wake.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- I. Howard Marshall. Luke: Historian and Theologian. Downers Grove, Illinois: InterVarsity Press.
- F.F. Bruce, The Speeches in the Acts of the Apostles. London: The Tyndale Press, 1942.[1] Ilihifadhiwa 31 Mei 2012 kwenye Wayback Machine.
- Helmut Koester. Ancient Christian Gospels. Harrisburg, Pennsylvania: Trinity Press International, 1999.
- Burton L. Mack. Who Wrote the New Testament?: The Making of the Christian Myth. San Francisco, California: HarperCollins, 1996.
- J. Wenham, "The Identification of Luke", Evangelical Quarterly 63 (1991), 3–44
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Biblical Interpretation of Texts of Saint Luke
- Early Christian Writings: Gospel of Luke e-texts, introductions
- National Academy of Sciences on Luke the Evangelist Ilihifadhiwa 9 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
- Gospel of Saint Luke in the Catholic Encyclopaedia
- Patron Saint Luke
- The Life of St. Luke the Evangelist, Apostle & Martyr Ilihifadhiwa 8 Septemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Gospel of St.Luke - Douay-Rheims Bible Ilihifadhiwa 12 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Photo of the grave of Luke in Padua (in German) Ilihifadhiwa 11 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- DNA testing of the Saint Luke corpse
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwinjili Luka kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |